Kwingineko

Al Hilal kufanya kufuru kwa Mbappe

IMERIPOTIWA  klabu ya Al Hilal ya Saudi Arabia imewasilisha dau la €300m kwa ajili ya mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe.

Ofa hiyo kutoka kwa matajiri hao wa uarabuni inakuwa ni ofa kubwa zaidi kuwahi kutokea katika soko la usajili ulimwenguni na ikiwa itakubaliwa na PSG itavunja rekodi inayoshikiliwa na Neymar ya kuwa mchezaji ghali zaidi ambapo mwaka 2017 alinunuliwa kwa dau la €222m kutoka Barcelona na kujiunga na PSG ya Ufaransa.

Sakata la Mbappe limepamba moto baada ya nyota huyo siku ya Ijumaa kuondoka kwenye kambi ya timu hiyo kutokana na sintofahamu  na klabu yake, tukio linalotafsiriwa kama safari ya kuondoka imewadia.

Related Articles

Back to top button