Kwingineko

Schmeichel kulinda mlango Anderlecht

GOLIKIPA wa zamani wa Leicester City ‘The Foxes’, Kasper Schmeichel amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuitumikia Anderlecht ya Ubelgiji.

Schmeichel mwenye umri wa miaka 36 amekuwa huru baada ya kuondoka Nice ya Ufaransa wiki iliyopita kwa makubaliano ya pande mbili ikiwa na maana anaweza kujiunga na klabu mpya nje ya dirisha la uhamisho.

“Anderlecht ni klabu kubwa. Kwa kweli nilitaka sana kuwa sehemu ya klabu hii,”amesema golikipa huyo wa Denmark.

Schmeichel amecheza mechi 46 msimu uliopita katika mashindano yote akiwa Nice baada ya kuijiunga na klabu hiyo ya Ligue 1 kwa uhamisho huru kutoka Leicester.

Golikipa huyo alicheza mechi 93 katika kipindi katika miaka 11 aliyodumu ‘Foxes’ ambako alishinda taji la Ligi Kuu England, Kombe la FA na Ngao ya Jamii.

Related Articles

Back to top button