AFCONAfrica

AFCON2023: Drone ‘yapeleleza’ mazoezi ya Algeria

HABARI zinasema ndege isiyokuwa na rubani (drone) imeruka katika eneo ilipokuwa ikifanya mazoezi timu ya taifa ya Algeria ‘The Fennec Foxes’ huko Ivory Coast ambako fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) zinanaza leo hivyo kutia hofu kwamba ilikuwa inapeleleza timu hiyo.

Kikosi cha The Fennec Foxes chenye wachezaji kama Riyad Mahrez, Rayan Ait-Nouri, Islam Slimani na Ismael Bennacer kipo katika maandlaizi ya mwisho kuwakabili wapinzani wake kundi.

Video za mitandao ya kijamii zimeonesha polisi wakimhoji mtu aliyekuwa akirusha ndege hiyo.

Hata hivyo mtandao wa michezo DZfoot umesema aliyekuwa akiirusha ndege hiyo ni raia wa Ivory Coast aliyeajiriwa na chombo cha habari za Algeria.

Algeria itacheza mechi tatu za makundi katika mji wa Bouaké ikianza Januari 15 dhidi ya Angola, kisha Januari 20 kuivaa Burkina Faso na kumaliza Januari 23 dhidi ya Mauritania.

Algeria inapewa kipaumbe cha nne kutwaa ubingwa wa AFCON nyuma ya Morocco, Senegal na mwenyeji Ivory Coast.

Related Articles

Back to top button