Muziki

Nandy siri ya Yammy kuacha kitovu nje

DAR ES SALAAM: Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Yammy amevunja ukimya na kujibu matusi aliyokuwa akipewa mitandaoni na mashabiki wa muziki juu ya aina ya mavazi anayovaa anapokuwa kwenye maeneo mbalimbali.

Yammy amesema kuwa anapovaa na kuacha kitovu wazi ni sehemu moja wapo ya yeye kujibrandi na kuweka watu wawe makini naye hivyo havai kwa kukosea bali yupo kimkakati zaidi.

Ameeleza kuwa alishauriwa na Boss wake Faustina Mfinanga ‘Nandy’ kuwa ni lazima ajiweke tofauti kama anataka kuliteka soko la muziki nchini.

Ameongeza kuwa hapo awali alikuwa akishindwa kuvaa hivyo lakini siku zilivyozidi kwenda amejikuta akizoea na sasa anaona ni jambo la kawaida kwake.

“Watu wasichokijua Boss wangu Nandy ndiye aliyenishauri kuvaa hivyo kwa sababu aliniambia nina umbo zuri na bado umri wangu ni mdogo hivyo nikivaa hivyo napendeza.”

“Nandy hawezi kuvaa hivyo kwa sababu umri wake na wangu ni tofauti na ukizingatia yeye ameshakuwa mama ana mtoto na ameolewa lakini kipindi cha nyuma akiwa na umri kama wangu ameshavaa sana.”amesema Yammy

Ikumbukwe Yammy sio msanii wa kwanza kuvaa hivyo kwani msanii kama Rachel Kizunguzungu (Ray C) pamoja na Mwanadada Judith Wambura Lady Jay Dee ni miongoni mwa wasanii waliokuwa wakiacha vitovu nje lakini umri ulivyosogea waliacha.

Related Articles

Back to top button