EPLKwingineko
Haaland mchezaji bora mwezi Agosti EPL

MSHAMBULIAJI Erling Haaland ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Agosti katika Ligi Kuu Uingereza(EPL) baada ya kung’ara mwanzo wa msimu wake Manchester City.
Tangu awasili Uingereza akitokea Borussia Dortmund, Ujerumani, Haaland amefunga mabao 9 katika michezo mitano mwezi wake wa kwanza katika EPL.
Alama hizo ni za juu zaidi kuwahi kufikiwa na mchezaji katika michezo mitano ya kwanza katika ligi hiyo na zimehusisha mabao matatu(hat-tricks) mara mbili mfululizo kwenye michezo ya City dhidi ya Crystal Palace na Nottingham Forest.
Ni Luis Suárez pekee ndiye aliyewahi kufunga mabao 10 katika kipindi cha mwezi mmoja Desemba 2013 katika historia ya Ligi Kuu Uingereza.