Habari Mpya

Tumedhamiria kuibuka na ushindi mkubwa zaidi-Kaze

KUELEKEA mchezo wa marudiano kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Zalan, Kocha msaidizi wa klabu hiyo Cedric Kaze amesema timu imejipanga kuhakikisha inaendeleza dozi dhidi ya miamba hiyo ya Sudan Kusini.

Mchezo huo utapigwa Septemba 17 uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza na Spotileo kocha huyo amesema mazoezi waliyofanya siku tatu na mchezo wa waligi dhidi ya Mtibwa Sugar vimewaimarisha wachezaji na kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wao wa kwanza dhidi ya Zalan.

“Ni mchezo ambao tumedhamiria kuibuka na ushindi mkubwa zaidi kuliko ilivyokuwa mchezo wa awali sababu tumerekebisha mapungufu yetu lakini pia tuliona njia waliyotumia kujilinda ambayo tumeipatia dawa,” amesema Kaze.

Mshambuliaji wa Yanga, Bernard Morrison.

Amesema jambo lingine zuri ni kurejea uwanjani kwa kiungo, Bernard Morrison ambaye alikosekana kwenye mchezo wa kwanza na ule wa ligi na anaweze kuwa sehemu ya mchezo huo.

Mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele.

Katika mchezo wa awali Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-0, huku mshambuliaji wake Fiston Mayele akifunga mabao matatu peke yake(hat-trick).

Related Articles

Back to top button