Habari Mpya
Simba Queens kundi A Ligi ya mabingwa Afrika wanawake
KLABU ya soka ya wanawake ya Simba imepangwa kundi A katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake iliyopangwa kuanza Oktoba 30 hadi Novemba 13, 2022, Morocco.
Makundi mawili ya michuano hiyo yamepangwa leo katika mji mkuu wa nchi hiyo, Rabat.
Simba Queens imepangwa kundi A pamoja na wenyeji ASFAR ya Morocco, Green Buffaloes ya Zambia na Determine Girls ya Liberia.
Kundi B lina mabingwa watetezi wa Mamelodi Sundowns Ladies ya Afrika Kusini, Bayelsa Queens ya Nigeria, Wadi Degla ya Misri na mwakilishi kutoka Muungano wa Mashirikisho ya soka Afrika ya Kati.
Simba imetinga michuano hiyo baada ya kutwaa ubingwa wa Kanda ya Baraza la Vyama vya soka Afika Mashariki na Kati(CECAFA).




