Africa

CAG azitaka Simba, Yanga fainali CAFCL

WAKATI homa ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika(CAFCL) ikizidi kupanda, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) Charles Kichere amezitakia heri Simba na Yanga zishinde michezo yao ili zisonge mbele.

Kichere amesema hayo leo Ikulu, Chamwino Dodoma wakati akikabidhi ripoti ya ofisi yake kwa Rais Samia Suluhu Hassan ya mwaka 2022/2023.

“Nomba nizitakie timu zetu za Simba na Yanga ushindi kwenye mechi zao za kesho na keshokutwa ili ziweze kushinda kwa kishindo nyumbani hivyo kuwa rahisi kwao kuingia nusu fainali na Mwenyezi Mungu akipenda baso timu hizi zikutane fainali,” amesema Kichere.

Simba itaikabili Al Ahly Machi 29 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa wakati Yanga itakuwa mwenyeji wa Mamelodi Sundowns Machi 30 kwenye uwanja huo huo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button