Man United yamwania kinda wa Everton

TETESI za usajili zinasema Manchester United inapanga beki wa England U21 anayekiwasha Everton Jarrad Branthwaite, 21, kuwa mlengwa wake wa usajili majira yajayo ya kiangazi.(Star)
Winga mfaransa wa Crystal Palace Michael Olise, 22, pia yumo kwenye orodha ya United ya usajili majira yajayo ya kiangazi. (Football Transfers)
United itasonga mbele na ombi la kumsajili Branthwaite, ambaye Everton inasema ana thamani ya pauni mil 75, bila kujali hatma ya kocha Erik ten Hag. (Mirror)
Everton ina nia kumsajili beki wa Hull City, Jacob Greaves, 23, ambaye anatarajiwa kuhamia Ligi Kuu England majira yajayo ya kiangazi iwapo klabu yake itashindwa kupanda daraja. (Football Insider)
Manchester City inaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Newcastle United na Brazil Bruno Guimaraes, 26, ambaye ana kipengele cha kuachiwa cha pauni mil 100 kwenye mkataba wake. (Football Transfers)