Tetesi

De Bruyne lulu Saudia

TETESI za usajili zinasema Manchester City inajiandaa kupokea ofa nzito kutoka klabu za Ligi ya kulipwa Saudi Arabia kumsajili kiungo wake Kevin De Bruyne majira yajayo ya kiangazi. (Mail)

Ili City ifikirie kumuuza De Bryune itahitajika ada ya pauni mil 100. (talkSPORT)

Manchester United ipo tayari kuhuisha kpengele cha kuachiwa cha pauni mil 85 katika mkataba wa mshambuliaji wa Sporting CP, Viktor Gyokeres, ambaye amefunga mabao 29 na kutoa pasi 11 za mabao katika michezo 32 aliyocheza hadi sasa msimu huu. (Fichajes – Spain)

Pia kiungo wa Fenerbahce, Sebastian Szymanski yupo kwenye rada ya Man Utd, ambaye pia anawindwa Arsenal na Tottenham. (TEAMtalk)

Chelsea inajiandaa kumuuza golikipa Robert Sanchez majira yajayo ya kiangazi na inaweza kuangalia uwezekano kumsajili Aaron Ramsdale toka Arsenal kuwa mbadala. (HITC)

Arsenal na Liverpool zinafukuzia saini ya kiungo wa Fulham, Joao Palhinha. (Football Insider)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button