Tetesi

Mmiliki Liverpool adhamiria kumsajili Mbappé

TETESI za usajili zinasema mmiliki wa klabu ya Liverpool John W. Henry yuko kwenye ‘dhamira binafsi’ ya kumsajili fowadi wa Paris Saint-Germain Kylian Mbappé.(Mundo Deportivo)

Huku wasiwasi ukizidi kuhusu nafasi ya Real Madrid kumsajili Mbappé, miamba hiyo ya Hispania inafikiria kuhamishia nia kwa mshambuliaji wa Manchester City, Erling Haaland.(AS)

Ombi la Arsenal la pauni mil 22 kumsajili Borja Mayoral wa Getafe limekataliwa. Mayoral, 26, amefunga mabao 12 Ligi Kuu Hispania, La Liga msimu huu.(Sun)

Barcelona itatafakari ofa kutoka nje kwa kila mchezaji katika kikosi chake mwisho wa msimu isipokuwa kwa Pedri, Gavi na Ronald Araujo ambao ni vipenzi vya kikosi cha Xavi.(Sport)

Kiungo wa Middlesbrough aliyefunga bao la ushindi dhidi ya Chelsea katika nusu fainali ya Kombe la Carabao, Hayden Hackney anazivutia Manchester United, Liverpool na Tottenham Hotspur.(Evening Standard)

Related Articles

Back to top button