Afrika Mashariki
Tanzania U15 moto CECAFA
TIMU ya soka ya taifa ya vijana chini ya miaka 15 leo imeshinda mchezo wa pili mfululuzo katika michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati(CECAFA) inayoendelea Uganda baada ya kuichapa Rwanda mabao 2-1.
Mchezo huo umefanyika uwanja wa kituo cha ufundi Njeru.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Novemba 5 Tanzania iliifunga Somalia bao 1-0.
FULLTIME
Rwanda 🇷🇼 U15 1️⃣-2️⃣ 🇹🇿Tanzania U15
Peter Andrew⚽️
Peter Andrew⚽️




