Ligi Daraja La Kwanza

Kane alitaka kwenda Man Utd

HARRY Kane alitaka kujiunga na Manchester United wakati mkataba wake Tottenham unakwisha 2024 na alikuwa anakusudia kufikia dili iwapo angehakikishiwa uhamisho kwenda Old Trafford.
Hata hivyo, badala yake aliishia kusaini Bayern Munich majira haya ya kiangazi.(Daily Mail)

Real Madrid ilituma ofa ya pauni milioni 60 Spurs ili kumsajili Kane na pia PSG ilikuwa na nia lakini Bayern Munich ilipata saini yake kwa dili lenye thamani ya pauni milioni 86.(The Athletic)

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy amethibitisha kuwa klabu hiyo ina chaguo la kumnunua Kane.(Evening Standard)

Manchester United pia ilitaka kumsajili Evan Ferguson majira haya ya kiangazi lakini Brighton & Hove Albion ‘imecheka’ ofa ya pauni milioni 50 iliyotumwa na United.(ESPN)

Youssoufa Moukoko hana furaha kutokana na muda anaopata kucheza Borussia Dortmud huku Barcelona na Chelsea zikijiandaa kutoa ofa kumsajili.(Fichajes)

Brentford inajiandaa kumuuza Ivan Toney huku Arsenal, Chelsea na Tottenham zikifikiria kumsajili mshambuliaji huyo wa England.(Daily Mirror)

Real Madrid inafirikia uhamisho wa ghafla wa Pierre-Emerick Aubameyang wa Marseille wakati wa dirisha dogo Januari 2024 katika juhudi za kuimarisha safu ya ushambuliaji. (Fichajes)

Chelsea iko tayari kutumia pauni milioni 35 kumsajili golikipa wa Valencia ya Hispania, Giorgi Mamardashvili huku klabu hiyo ya Uhispania ikiona mauzo ya mchezaji huyo kuwa ni nafasi maalumu ya kibiashara.(Fichajes)

Related Articles

Back to top button