Kwingineko

Anthony yamemkuta United

MANCHESTER United imesema inachukulia kwa uzito madai yaliyotolewa dhidi ya winga Antony Matheus dos Santos maarufu Antony baada ya kutuhumiwa kumnyanyasa mpenzi wake wa zamani.

Mtandao wa habari UOL wa Brazil ulichapisha madai hayo ya mpenzi wa zamani wa Anthony Sepemba 4.

Polisi wa Sao Paulo, Brazil na Greater Manchester, England wanachunguza tuhuma hizo ambazo mchezaji huyo amekanusha.

Anthony mwenye umri wa miaka 23 ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Brazil baada ya habari za madai hayo kufichuka.

United imesema: “Manchester United inakiri madai yaliyotolewa dhidi ya Antony na inabainisha kuwa polisi wanafanya uchunguzi. Wakati klabu inasubiri taarifa zaidi, haitatoa kauli zaidi.”

Kupitia mitandao ya Kijamii Anthony amesema: “Ninaweza kusema kwa utulivu kwamba shutuma hizo ni uongo na kwamba ushahidi ambao tayari umetolewa na mwingine utakaotolewa unaonesha kwamba sina hatia katika shutuma hizo.”

Antony anashutumiwa kwa kumshambulia mpenzi wake wa zamani Gabriela Cavallin “kwa kumpiga kichwa” kwenye chumba cha hoteli jijini Manchester Januari 15, 2023 na kusababisha majeraha kichwani ambayo yalihitaji matibabu.

Idara ya Polisi ya Greater Manchester imesema inatambua madai hayo na uchunguzi bado unaendelea kugundua mazingira ya ripoti ya tuhuma hizo na kwamba haitatoa maelezo yoyote kwa wakati huu.

Related Articles

Back to top button