Kwingineko

Sancho kwenda Juventus? De Ligt kutua United

CHELSEA wanazungumza na Borussia Dortmund kuona uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Kijerumani, Karim Adeyemi, 22. (Bild–in-Germany).

West Ham wanavutiwa na mshambuliaji wa Aston Villa, Jhon Duran, 20. (Sky Sports).

Manchester United wamekubaliana na Bayern kuhusu uhamisho wa beki wa Bayern Munich, Matthijs de Ligt mwenye umri wa miaka 24. (Manchester Evening News).

Klabu ya Juventus bado ina nia ya kumsajili winga wa Manchester United Muingereza Jadon Sancho, 24. (Sky Sports).

Nottingham Forest na Wolves wanavutiwa na mlinzi wa Le Havre Mfaransa Etienne Youte Kinkoue, 22. (Football Insider).

Baadhi ya mashabiki wa Marseille wameitaka klabu hiyo kusitisha nia yake ya kumnunua mshambuliaji wa Manchester United Muingereza Mason Greenwood, 22. (Mirror).

Winga Nico Williams, 21, anayevutuiwa na Liverpool, Chelsea, Bayern Munich na Barcelona, ana kipengele cha kutolewa cha Euro milioni 55 katika mkataba wake Athletic Bilbao. (Marca).

Beki wa Sweden Victor Lindelof, 29, anaweza kuondoka Manchester United msimu huu wa joto kwa sababu ya kukosa nafasi misimu miwili iliyopita. (Givemesport ).

Related Articles

Back to top button