World Cup

Mpinzani wa Man City Kombe la Dunia la Klabu huyu hapa

Manchester City itaikabili klabu ya Leon ya Mexico au Urawa Reds ya Japan katika mechi yake ya ufunguzi ya michuano ya Kombe la Dunia la Klabu.

City imefuzu michuano hiyo kwa mara ya kwanza baada ya kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya 2022-23 na itaanza kampeni yake hatua ya nusu fainali.

Timu ya Leon ni mabingwa watetezi wa taji la Shirikisho la Vyama vya Soka Amerika ya Kaskazini, Kati na Caribbean(Concacaf) na Urawa Reds ni ilishinda Ligi ya Mabingwa Asia(AFC).

Mashindano hayo ya Kombe la Dunia la Klabu yatafanyika katika jiji la Jeddah, Saudi Arabia kati ya Desemba 12 na 22 mwaka huu yakishrikisha timu saba.

Related Articles

Back to top button