Lukaku kutua Spurs

TOTTENHAM Hotspur inafikria kumsajili Romelu Lukaku lakini iwapo itawezekana kwa mkopo.
Mbelgiji huyo amekuwa kama amesahaulika Stamford Bridge licha kusajiliwa kwa rekodi ya ada ya pauni milioni 97.5 sawa na shilingi bilioni 298.8 miaka miwili tu iliyopita.
Lukaku ameitumikia Inter Milan msimu uliopita kwa mkopo na alitarajiwa kuondoka rasmi.
Lukaku amekuwa akifanya mazoezi peke yake tangu arejee Chelsea huku kocha Mauricio Pochettino akiweka wazi kuwa mchezaji huyo hatakuwa kwenye mipango ya klabu kwa ajili ya kampeni ya sasa.
Hata hivyo, kulingana na ripoti ya mtandao wa michezo Tutto Mercato wa Italia, fowadi huyo wa kibelgiji bado anaweza kucheza Ligi Kuu England msimu huu.
Tutto Mercato imedai kwamba Spurs ina nia kumsajili Lukaku kwa mkopo huku Mwenyekiti wa klabu hiyo Daniel Levy akiwa hataki kukubali ada ya kudumu kwa mshambuliaji huyo ambaye tayari ana miaka 30.