Al-Nassr yamtupia macho Álisson

KLABU ya Al-Nassr inayoshiriki Ligi ya kulipwa ya Saudi Arabia imeripotiwa kuwa na nia kubwa kumsajili golikipa wa Liverpool, Álisson Ramsés Becker.
Kwa mujibu wa mtandao wa michezo wa Footmercato mbrazil huyo anajaribiwa na uwezekano wa kuhamia nchi hiyo ambako Jordan Henderson, Fabinho, na Roberto Firmino wamesajiliwa majira haya ya joto kutoka Liverpool.
Al-Nassr hairidhishwi na kiwango cha golikipa wake kufuatia kipigo cha hivi karibuni cha mabao 2-1 kutoka kwa Al-Ettifaq inayonolewa na Steven Gerrard.
Sasa klabu hiyo inataka Álisson mwenye umri wa miaka 30 achukue nafasi ya golikipa huyo, Nawaf Al-Aqidi.
Álisson, ambaye amecheza mechi 232 Liverpool tangu ajiunge nayo mwaka 2018 kwa ada ya pauni milioni 65 sawa na shilingi bilioni 208.6 anaweza kuwa nyota wa hivi karibu kuhamia Saudi Arabia iwapo ataamua kundoka Anfield.