
PAZIA la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2023/2024 linafunguliwa leo kwa michezo mitatu kupigwa Dodoma, Lindi na Mbeya.
‘Walima zabibu’ Dodoma Jiji watafungulia msimu kwa kuwakaribisha ‘Wanamangushi’ Coastal Union ya Tanga kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Nyasi za Uwanja wa Majaliwa mkoani Lindi zitawaka moto wakati wageni wa ligi JKT Tanzania itakapowakabili wenyeji Namungo ‘Wauaji wa Kusini’.
Mkoani Mbeya, klabu ya Ihefu ‘Mbogo Maji’ itawakaribisha ‘Matajiri wa dhahabu’, Geita Gold kwenye uwanja wa Estates Highland uliopo Mbarali.