Nyumbani

Coastal kujipima dhidi Bandari

KLABU ya Coastal Union itacheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Bandari ya Kenya mkoani Tanga Julai 29.

Mchezo huo ni wa kwanza wa maandalizi kwa Wanamangushi hao kuelekea msimu mpya wa mashindano 2023/2024.

“Kesho tutakuwa na mchezo wa kimataifa wa kirafiki katika Uwanja wa Mkwakwani tukiikaribisha timu ya Bandari ya Mombasa Kenya saa 10:00 jioni kwa kiingilio cha Tsh 2000/ Tu,” imesema Coastal kupitia mitandao yake ya kijamii.

Tayari Coastal imesajili wachezaji wapya wawili Lucas Kikoti na Ally Kombo huku ikimteua Mwinyi Zahera kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo.

Related Articles

Back to top button