Ashley Young atua Everton, kufanyiwa vipimo leo
BEKI Ashley Young amekubali kujiunga na Everton na anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya leo baada ya kuondoka Aston Villa majira haya ya joto akiwa mchezaji huru.
Ripoti zimesema mkataba wa Young Villa Park ulimalizika na alifanya mazungumzo na klabu ya Luton huku kukiwa pia na klabu ya Saudi Arabia ikihitaji huduma yake.
Young mwenye umri wa miaka 38 alishinda makombe ya Ligi Kuu na FA England akiwa na Manchester United na pia taji la Serie A akicheza Inter Milan.
Usajili wa beki huyo wa kwanza wa Everton chini ya Kocha Sean Dyche.
Doyche bosi wa zamani wa Burnley alichukua mikoba Januari 2023 kutoka kwa Frank Lampard aliyetimuliwa na kuiongoza Everton kusalia EPL katika siku ya mwisho ya msimu uliopita.
Young aliyekuwa akicheza nafasi ya winga alishinda Ligi ya Europa na Kombe la Ligi akiwa United na amecheza mechi 39 timu ya taifa England.
Amecheza michezo zaidi ya 700 katika klabu na England ikimwemo 32 akiwa Villa msimu uliopita.




