Tetesi

Barca yafukuzia saini ya kinda Güler

RAIS wa Barcelona ‘Blaugrana’ Joan Laporta amefichua kuwa Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo Anderson Luís de Souza OIH ‘Deco’ amekwenda jijini Istanbul, Uturuki kufanya oparesheni ya uhamisho wa kiungo mshambuliaji machachari Arda Güler.

Kwa mujibu gazeti la kila siku, Mundo Deportivo la michezo la Hispania, kinda huyo wa Fenerbahçe anawindwa na vilabu kadhaa vikubwa Ulaya kufuatia kiwango bora anachoonesha.

Akifikiriwa kuwa moja ya vipaji bora zaidi Ulaya, Güler ana kipengele cha kuachiwa chenye thamani ya Euro milioni 18.5 sawa na shilingi bilioni 47.3 katika mkataba wake wa sasa ambacho kinaweza kutekelezwa majira haya ya joto.

Imeripotiwa kuwa Real Madrid imekuwa katika mpango wa kumshawishi Güler mwenye umri wa miaka 18 pamoja na vilabu vingine vikiwemo Arsenal, Liverpool, Newcastle United, Paris Saint-Germain, AC Milan na Sevilla.

Hata hivyo, inaonekana kana kwamba Barca imevipita vilabu hivyo katika mbio za uhamisho huku Laporta akieleza kwamba makubaliano yanaweza kufanyika hivi karibuni.

“Leo Deco amekwenda Istanbul. LaLiga imeturuhusu kufanya uhamisho kwa ajili ya msimu ujao bila kuathiri mchezo wa haki. Arda Güler ni mchezaji mwenye kipaji, ambaye Deco anampenda na tunajaibu kukamilisha uhamisho,” amesema Laporta.

Hata hivyo Rais huyo wa Blaugrana ameongeza kuwa uhamisho wa Güler umepangwa kufanyika mwaka ujao ikiwa na maana kinda huyo wa Kituruki atabaki Fenerbahçe kwa mkopo hadi kipindi hicho.

Güler anafananishwa na mkongwe wa Barca na mshindi wa Kombe la Dunia muajentina Lionel Messi kutokana na mtindo wa uchezaji wake.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button