Ligi KuuNyumbani

Gadiel Michael wa saba kupewa ‘Thank You’

MLINZI Gadiel Michael leo amekuwa mchezaji wa saba kuachana na klabu ya Simba.

Taarifa ya Simba imesema Gadiel imepewa ‘Thank You’ kutokana na mkataba kufikia mwisho.

“Uongozi wa klabu unapenda kuwajulisha kuwa hatutaendelea kuwa na mlinzi wa kushoto Gadiel Michael baada ya mkataba wake kufikia tamati,” imesema taarifa ya Simba.

Wachezaji wengine waliokwishapewa ‘Thank You’ Simba ni Mohamed Ouattara, Nelson Esor-Bulunwo Okwa, Victor Akpan, Beno Kakolanya, Jonas Mkude na Erasto Edward Nyoni.

Related Articles

Back to top button