Kwingineko

Wamiliki Chelsea wanunua hisa RC Strasbourg

WAMILIKI wa timu ya Chelsea ‘The Blues’, BlueCo, wamekuwa wanahisa wapya wa klabu ya RC Strasbourg ya Ufaransa iliyomaliza nafasi ya 15 Ligue 1.

Chini ya vipengele vya dili hilo Rais wa Strasbourg, Marc Keller ambaye aliwahi kuwa mchezaji wa West Ham, Portsmouth na Blackburn za England kati ya mwaka 1998 na 2002 atabaki katika nafasi hiyo.

“Hii ni siku muhimu kwa Racing. Ni jambo ambalo mimi na marafiki zangu wanahisa tulikuwa tukilifikiria kwa karibu miaka miwili iliyopita,” amesema Keller.

Chelsea haijazungumzia kiwango cha hisa hizo lakini ripoti kutoka Ufaransa zimedai kuwa wamiliki wa The Blues wamenunua klabu nzima kwa karibu pauni milioni 65 sawa na shilingi bilioni 193.6.

BlueCo ni kampuni mama iliyoanzishwa na Todd Boehly na Clearlake Capital iliyoinunua Chelsea msimu uliopita.

Related Articles

Back to top button