Mwanamuziki mpiga gitaa mahiri ya solo na rithimu, Adolf Nicholaus Mbinga, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Taarifa ya kifo cha mwanamuziki huyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania (CHAMUDATA).
Marehemu atakumbukwa kwa upigaji wake mahiri wa gitaa na utunzi wa nyimbo nyingi maarufu akiwa na bendi mbalimbali.
Nyimbo hizo ni pamoja na Neema akiwa na bendi ya Diamond Sound (Dar es Salaam Kibinda Nkoy), Kisa cha Mpemba, Bwana Kijiko, na Tabu za Maisha akiwa na bendi ya African Stars (Twanga Pepeta), Tabu za Maisha Rremix, Binadam na Mto wenye Mamba akiwa na bendi ya Mchinga Sound, na Betty wa Mwanamuziki Juma Kakere.
Katika uhai wake Mbinga aliwahi pia kufanya kazi na bendi za Mlimani Park Orchestra (Sikinde Ngoma ya Ukae) na Orchestra Sikinde Original.




