EPL

United yapewa sharti kwa Sabitzer

MANCHESTER United imepewa sharti na Bayern Munchen la kutoa Pauni milioni 22 endapo inataka kumsajili Marcel Sabitzer kwa mkataba wa kudumu.

Sabitzer ,29, ambaye anakipiga United kwa mkopo, mwishoni mwa msimu huu anatakiwa kurejea Bayern, hivyo inaonekana kama timu hiyo imekusudia kumuachia Muastria huyo.

Licha ya kuwa majeruhi, na kutumika kwa kipindi kifupi tangu mwezi Januari, United inaonesha kuwa imeridhishwa na uwezo wa kiungo huyo.

Sabitzer tayari ameisaidia United kushinda ubingwa wa Carabao Cup na kuipelekea timu hiyo fainali ya Kombe la ‘FA’.

Related Articles

Back to top button