EPL
Arsenal yampa maisha Ramsdale

ARSENAL imemuongezea mkataba wa miaka mitano nyanda wao, Aaron Ramsdale, utakaomuweka klabuni hapo hadi 2028.
Kipa huyo amesaini ikiwa ni mwendelezo wa timu hiyo kuongeza mikataba kwa wachezaji watakaoendelea kukijenga kikosi hicho kwa msimu ijayo.
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amesema: “ni hatua nzuri ya kuendelea kujenga kikosi chetu, kwa wachezaji wenye vipaji, kwa timu yetu ya vijana.” amesema Arteta.
Ramsdale alijiunga na Arsenal mwaka 2021 akitokea Sheffield United. Kipa huyo sasa anawania tuzo ya kipa bora wa Ligi Kuu England.