Ligi Ya Wanawake
Kocha Fountaine Gate Princess ubingwa bado

KOCHA Mkuu wa Fountain gate Princess, Juma Masoud amesema mchezo wa leo dhidi ya JKT Queens utatoa taswira ya mbio za ubingwa wa ligi hiyo ambayo kivumbi cha ubingwa kimeshika kasi kwasasa.
Kocha Masoud anasema ushindi dhidi ya JKT Queens umebeba hatma ya mbio za ubingwa lakini anakiri ugumu wa mtanange huo
“Vijana wangu wapo katika ari nzuri, japokuwa mchezo utakuwa mgumu sana kwasababu tunacheza na timu ambayo haijafungwa mpaka sasa kwenye ligi”
Mpaka sasa Fountain Gate wana alama 38 katika nafasi ya tatu kwenye ligi hiyo wakati Jkt Queens wao wapo kwenye nafasi ya pili wakiwa na alama 40 alama mbili nyuma ya vinara Simba Queens waliocheza mchezo mmoja zaidi.