MastaaMitindo

Msanii matatani akidaiwa kubaka

MSANII wa ubunifu wa kuchora tattoo, Paul Marealle amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shtaka la ubakaji.

Msanii huyo amesomewa mashitaka mahakamani hapo na Wakili wa Serikali, Yusuph Aboud mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Pamela Mazengo.

Katika shitaka hilo, Marealle anadaiwa kumbaka msanii mwingine wa fani ya maigizo (jina limehifadhiwa), akiwa hajitambui baada ya kumwekea dawa za kulevya.

Ilidaiwa kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Novemba 9, 2018 katika eneo la Makongo Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam.

Aboud alidai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na aliomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba mosi, 2022 na mshitakiwa amepelekwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana, ikiwemo kupeleka wadhamini wawili wenye utambulisho.

Related Articles

Back to top button