Nyumbani
Patashika Kiluvya vs TANESCO Ligi mikoa leo

FAINALI za Ligi ya Mabingwa wa Mikoa 2023 zinaendelea leo mkoani Kilimanjaro kwa michezo miwili ya kundi A.
Katika mchezo wa awali Annuary ya Shinyanga itakumbana na Tanzania Navy ya Dar es Salaam kwenye uwanja wa Majengo mjini Moshi.
Mtanange wa pili utazikutanisha Kiluvya ya Dar es Salaam na TANESCO ya Kilimanjaro kwenye uwanja huo huo.