
MCHEZO wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga uliochezwa Aprili 16 umeingiza sh milioni 410.6.
Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imesema mashabiki 53,569 waliingia wakati wa mchezo huo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
TFF imesema timu mwenyeji ambayo ni Simba imepata sh milioni 188.987. Simba ilishinda mchezo huo kwa mabao 2-0.