Ligi Daraja la Kwanza wanawake Apr 12

LIGI Daraja la Kwanza Wanawake(WFDL) msimu wa 2022-2023 inatarajiwa kuanza Aprili 12 hadi 25, 2023 katika viwanja vya Shule ya Alliance jijini Mwanza.
Taarifa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imesema wachezaji wanaoruhusiwa katika ligi hiyo ni wale ambao hawakusajiliwa kucheza Ligi Kuu ya Wanawake(2022-2023) ambao usajili wao umepitishwa na TFF.
Timu zitakazoshiriki WFDL na mikoa zinakotoka ni Bilo(Mwanza), TSC Queens(Mwanza), Ukerewe(Mwanza), Bunda Queens(Mara), Geita Gold Queens(Geita), Singida Warriors(Singida), Allan Queens(Singida) na Mt Hanang Queens(Manyara).
Nyingine ni Lengo Queens, Mlandizi Queens(Pwani), Ilala Queens(Dar es Salaam), JMK Park Queens(Dar es Salaam), Masala Queens(Dar es Salaam), Oysterbay Queens(Dar es Salaam) Ruangwa Queens(Lindi) na Mapinduzi Queens(Njombe).
TFF imesema timu mbili za juu ztapanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite(SLWPL) msimu wa 2023-2024.