Ligi KuuNyumbani

Bruno asema anataka kuacha historia Singida

KIUNGO wa Singida Big Stars, Bruno Gomes amesema anataka kuonesha juhudi kwa kusaidia timu yake kumaliza Ligi Kuu Tanzania Bara katika nafasi za juu ili kuacha historia
itakayomfanya kukumbukwa popote aendapo.

Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na Yanga na anatajwa huenda msimu ujao akajiunga nao katika dirisha kubwa la usajili.

Akizungumza na gazeti la HabariLEO mchezaji huyo amesema anatamani kuiona timu yake inapata mafanikio na tetesi juu yake kwamba amefuatwa na Yanga sio za kweli, amejikita namna gani ya kusaidia timu yake kufikisha malengo yaliyokusudiwa.

“Hakuna timu yoyote iliyonifuata kutaka huduma yangu, ninachotamani kwa sasa ni kufanya kazi kwa bidii na kuisaidia Singida kuwa katika nafasi ya juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu na kulikuza jina la Singida Big Stars,” amesema.

Mchezaji huyo amekuwa akifanya vizuri akiwa ameifungia timu yake mabao tisa na ni miongoni mwa wachezaji wanaoongoza katika ufungaji bora.

Singida Big Stars imekuwa ikifanya vizuri msimu huu inashika nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo 25 na kati ya hiyo, imeshinda 14, sare sita na kupoteza mitano ikifikisha pointi 48.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button