AfricaAfrika Mashariki

Vipers yamtimua Bianchi

KLABU ya Vipers ya Uganda imetangaza kuvunja mara moja mkataba na Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Beto Bianchi siku 58 tu baada ya kumtambulisha.

Mchezo wa mwisho wa Kocha Bianchi akiwa na timu hiyo ya Kampala, ilipoteza mchezo kwa goli 1-0 dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Klabu ingependa kumshukuru Bianchi kwa juhudi zake zake wakati akiwa klabuni hapa na kumtakia mafanikio katika majukumu yake mapya,” imesema taarifa ya Vipers.

Biachi alitambulishwa kuwa Kocha Mkuu mpya wa Vipers Januari 10, 2023 baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Roberto ‘Robertinho’ Oliviera kuhamia Simba.

Related Articles

Back to top button