Kocha Amrouche atambulishwa

Waziri wa Utamaduni, Sana na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali inaamini Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limejiridhisha kuwa Adel Amrouche ni Kocha Bora atakayekuza soka la Tanzania.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati wa hafla ya kumtambulisha Kocha huyo mpya wa Taifa Stars leo jijini Dodoma Balozi Dkt Chana amesema katika kuendeleza mchezo wa soka nchini itamlipa mshahara Amrouche ambaye ni raia wa Ubelgiji mwenye asili ya Algeria.
” Ukitazama wasifu wa Kocha Adel utabaini uzoefu mkubwa alionao sio tuu katika kufundisha soka uwanjani, bali pia katika kuandaa wataalamu wengine wa soka, hivyo tumtumie vizuri ili asaidie timu yetu kufanya vizuri ndani na nje ya nchi,”amesema Balozi Dkt Chana.

Kwa upande wake Kocha Amrouche ameahidi kuwanoa wachezaji vyema ili kuiweka juu zaidi Tanzania katika ulimwengu wa soka, huku akisisitiza ushirikiano kutoka kwa wadau mbalimbali katika kufanikisha kazi yake.