Africa

Samia kutoa mil 5/- kila goli Simba, Yanga

RAIS Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa Sh milioni 5 kwa kila goli litakalofungwa na wachezaji wa timu za Simba na Yanga wakati wa michezo inayofuata ya Ligi ya Mabingwa  na Kombe la Shirikisho Afrika.

Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema hayo Dar es Salaam leo wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari.

Simba itakutana na vinara wa kundi C, Raja Casablanca katika dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Februari 18, 2023 wakati Yanga iliyopo kundi D itakuwa mwenyeji wa TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Februari 19, 2023.

Yanga iliambulia kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa US Monastir ya Tunisia Februari 12 wakati Simba ilifungwa bao 1-0 na Horoya ya Guinea mjini Conakry, Februari 11.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button