Ligi Ya WanawakeNyumbani
Amani Queens vs Alliance Girls kupimana ubavu leo

LIGI ya Kuu ya Soka ya wanawake Tanzania Bara (SLWPL) inaendelea kwa mchezo mmoja kupigwa mkoani Lindi.
Katika mchezo huo Amani Queens itakuwa wenyeji wa Alliance Girls kwenye uwanja wa Ilulu.
Alliance Girls ipo nafasi ya 6 katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa pointi 10 baada ya michezo 7 wakati Amani Queens ni ya 9 ikiwa na pointi 4.