Filamu ya Ramayana yawaliza Wasweeden

SWEEDEN: MUIGIZAJI mkongwe wa Bollywood, Anupam Kher, amesema amejawa na furaha na fahari kuiona India ikipata heshima kupitia filamu ya Ramayana, baada ya watazamaji nchini Sweden kuguswa kihisia na simulizi ya filamu hiyo.
Kher ameeleza kuwa watazamaji walionesha hisia kali wakati wa kuitazama filamu hiyo, huku baadhi yao wakishindwa kujizuia kulia kutokana na matukio yaliyowasilishwa katika simulizi hiyo.
Muigizaji huyo amesema baada ya filamu kumalizika, watazamaji walimfuata na kumshukuru kwa mchango wake katika kazi hiyo, hasa kwa kutoa sauti ya mhusika Jatayu.
Amesema tukio hilo lilimgusa sana kwa sababu hakutarajia kuona watazamaji wa nchi nyingine wakiguswa kwa kiwango hicho na simulizi inayotokana na utamaduni wa India.
Kwa mujibu wa Kher, mapokezi hayo ni ishara kuwa sanaa na simulizi zenye ujumbe mzito zina uwezo wa kuvuka mipaka ya lugha, tamaduni na mataifa na kuwafikia watu wa sehemu mbalimbali duniani.
Kauli yake imeongeza mjadala kuhusu mafanikio ya Ramayana na namna filamu hiyo inavyoendelea kuitangaza historia na utamaduni wa India kimataifa kupitia tasnia ya burudani.




