Muziki

Leyla ampongeza Isha kutimiza miaka 20

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Taarabu, Leyla Mzee Yusuph, amempongeza mwimbaji mwenzake, Isha Mashauzi, kwa juhudi na bidii yake katika muziki huo, akieleza kufurahishwa kwake kuwa sehemu ya hafla ya kuadhimisha miaka 20 ya Isha katika muziki wa Taarabu.

Leyla amesema “Nazipenda nyimbo za Isha Mashauzi na kumpongeza kwa kuendelea kupambana na kufanya kazi kwa bidii katika safari yake ya muziki.

Amesema “Isha ni mwanamke mwenye juhudi na anayejikita zaidi katika kufanya kazi badala ya kupoteza muda kwenye maneno yasiyo na tija kwake wala kwa watu wengine.

Aidha, Leyla ameeleza kufurahishwa kwake kushiriki katika hafla hiyo muhimu, akimtakia Isha mafanikio zaidi na kuendelea kufanya vizuri katika muziki wa Taarabu.

Katika hatua nyingine, Leyla ametoa wito kwa vyombo vya habari, hususan vituo vya redio na televisheni, kuongeza nafasi ya kucheza nyimbo za Taarabu ili kuupa muziki huo nguvu na kuurudisha katika hali yake ya umaarufu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya wasanii na vyombo vya habari ni muhimu katika kuendeleza muziki wa Taarabu, kuwafikia mashabiki wengi zaidi na kuhakikisha unaendelea kuwa sehemu muhimu ya burudani nchini.

Related Articles

Back to top button