Nyumbani

Simba kufanya mkutano mkuu Januari 3

DAR ES SALAAM: BODI ya Wakurugenzi ya Simba imetangaza kuwa mkutano mkuu wa kawaida wa mwaka 2026 pamoja na uchaguzi wa viongozi wa klabu hiyo utafanyika Januari 3, 2027 jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na bodi hiyo jana, imeeleza kuwa mkutano huo utafanyika kwa mujibu wa Katiba ya Simba ya mwaka 2018, Toleo la 2026, huku wanachama wakitakiwa kujiandaa kushiriki.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wito rasmi wa mkutano, ajenda pamoja na nyaraka nyingine zinazohusiana na mkutano huo zitawasilishwa kwa wanachama kupitia matawi yao.

Bodi hiyo imewataka wanachama wote kujiandaa kuhudhuria mkutano huo ambao, pamoja na mambo mengine yatakayobainishwa katika ajenda rasmi, utaambatana na uchaguzi wa viongozi wa klabu hiyo.

Uamuzi huo unakuja wakati Simba ikiendelea na shughuli zake za kimashindano, huku mkutano huo ukitarajiwa kuwa sehemu muhimu ya masuala ya uongozi na mustakabali wa klabu hiyo.

Simba inaingia katika kipindi hicho ikiwa na mafanikio ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuiondosha 15 de Agosto ya Guinea ya Ikweta katika hatua za awali za mashindano hayo.

Related Articles

Back to top button