
MSHAMBULIAJI Adam Adam amejiunga na klabu ya Ihefu ya Mbarali mkoani Mbeya akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.
Adam amesajiliwa Ihefu baada ya kufikia makubaliano na Mtibwa Sugar kuvunja mkataba wake wa miezi sita uliokuwa umesalia.
Adam Adam pia amewahi kucheza klabu ya Al Wahda ya Libya.