Mastaa

Ayra Starr: Nikikutana na mwenye mvuto zaidi, navunja uhusiano wangu

LAGOS: MWANAMUZIKI wa Nigeria, Ayra Starr ameshtua umma baada ya kusema atavunja uhusiano wake wa mapenzi endapo atakutana na mwanaume mwingine anayemvutia zaidi.

Mkali huyo wa ngoma ya Heaven Baby, alieleza hayo alipokuwa akijibu swali la shabiki yake wa kike kwenye kipindi cha Ask Ayra Starr.

Shabiki huyo alimweleza Ayra hali aliyonayo sasa kwamba kuna mwanaume mwingine anamvutia zaidi ya aliyenaye sasa, hivyo afanyaje, ndipo Ayra akayoosha maelezo juu ya hilo.

“Kama niko katika uhusiano mzito na mwanaume kisha nikakutana na mwanaume mwingine anayevutia zaidi, ningeachana naye badala ya kuwa na uhusiano na wote wawili kwa wakati mmoja. Sidhani kama unaweza kuwapenda watu wawili, nadhani unahitaji muda wako binafsi ili uweze kutafakari na kufanya uamuzi,” alisema.

Akijibu swali lingine, Ayra aliwashauri pia mashabiki wake kutowatelekeza marafiki zao kwa sababu tu wako kwenye uhusiano wa kimapenzi.

Alisisitiza kuwa kunapaswa kuwa na uwiano kati ya urafiki na uhusiano wa kimapenzi.

“Hupaswi kamwe kuwatelekeza marafiki zako kwa sababu uko kwenye uhusiano wa kimapenzi. Mpenzi wako hapaswi kukutenganisha na marafiki zako kwa sababu tu mko pamoja. Kunapaswa kuwe na uwiano kati ya urafiki na uhusiano wa kimapenzi,” alifafanua.

 

Related Articles

Back to top button