Azam FC wako tayari kuikabili Coastal Union

DAR ES SALAAM: KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Kassim Liogope, amesema kikosi chake kipo tayari kuikabili Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu, baada ya kupata muda wa kutosha kujiandaa wakati wa mapumziko ya ligi.
Liogope amesema muda walioupata katika maandalizi umewasaidia kuwajenga wachezaji kuelekea mchezo huo, huku akisisitiza umuhimu wa timu kutumia maandalizi hayo kupata matokeo mazuri.
“Wachezaji wako tayari dhidi ya Coastal Union. Tunashukuru tumepata muda wa maandalizi, tumejiandaa vizuri kwa kucheza michezo miwili ya kirafiki, wachezaji waliokuwa timu ya taifa pia wamerejea, wote wako imara,”amesema.
Kwa upande wake, beki wa Azam FC, Lusajo Mwaikenda, amesema anaamini mchezo huo utakuwa mzuri na kwamba wachezaji wapo tayari kupambana kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu.
“Naamini mchezo wa Coastal Union utakuwa mzuri sana na tuko tayari kupambana ili kupata pointi tatu,” amesema.




