Muziki

Jaguar arejea kwenye muziki baada ya miaka mitatu

NAIROBI: MWANAMUZIKI maarufu kutoka Kenya, Charles Njagua maarufu kama Jaguar, amerejea kwenye muziki baada ya kukaa kimya kwa takribani miaka mitatu, ambapo metoa wimbo mpya uitwao ‘Safari ya Maisha.’

Jaguar ameachia wimbo huo ikiwa ni hatua yake ya kurejea rasmi kwenye anga la muziki baada ya kazi yake kubwa ya mwisho, ‘Unthinkable,’ aliyoshirikiana na mwanamuziki wa Tanzania, Lava Lava.

Akizungumza kuhusu wimbo huo, Jaguar amesema ameuandaa kwa lengo la kuwapa matumaini watu wanaopitia changamoto mbalimbali katika maisha na kuwakumbusha kuwa hawapaswi kukata tamaa.

Jaguar amesema ‘Safari ya Maisha’ pia inaelezea sehemu ya maisha yake, ikiwemo kukua katika mazingira magumu na kumpoteza mama yake akiwa bado mdogo.

Kupitia wimbo huo, msanii huyo anaeleza namna changamoto hizo zingeweza kuvuruga ndoto zake, lakini aliamua kuendelea kusonga mbele na kufuatilia ndoto yake ya kuwa mwanamuziki.

Baada ya juhudi hizo, hatimaye alifanikiwa kujijenga katika tasnia ya muziki nchini Kenya na kuwa miongoni mwa wasanii waliotambulika zaidi nchini humo.

Related Articles

Back to top button