Mosimane aionya Afrika Kusini kabla ya kuikabili Kenya

AFRIKA KUSINI: KOCHA Pitso Mosimane ameonya kuhusu ushindani mkubwa unaolikabili Afrika Kusini katika Kundi D la kufuzu AFCON 2027, baada ya Kenya kuwa tayari imepata nafasi ya kushiriki michuano hiyo kama mwenyeji mwenza.
Mosimane amesema hali hiyo imeifanya nafasi iliyobaki ya kufuzu kuwa ya ushindani mkubwa, kwani mataifa mengine yaliyopo kwenye kundi hilo yanapambana kugombea tiketi moja iliyosalia.
Akizungumza kabla ya mchezo muhimu kati ya Afrika Kusini na Kenya, Mosimane amesisitiza kuwa kila pointi itakuwa na umuhimu mkubwa katika mbio hizo za kufuzu.
Amesema pia kila bao na matokeo ya michezo ya moja kwa moja kati ya timu zinazowania nafasi hiyo yanaweza kuwa na umuhimu mkubwa pale itakapofika hatua ya kuamua timu itakayopata tiketi ya mwisho.
Tanzania tayari imehakikisha nafasi yake AFCON 2027 kutokana na kuwa mwenyeji mwenza pamoja na Kenya na Uganda kupitia zabuni ya pamoja.
Kwa hali hiyo, ushindani wa Kundi D umebaki kuwa wa juu kwa timu nyingine, huku Afrika Kusini ikilazimika kuweka nguvu katika kila mchezo ili kutengeneza nafasi ya kufuzu AFCON 2027.




