Nyumbani

Feisal bado mchezaji Yanga-TFF

KAMATI ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imeamua kuwa Feisal Salum bado ni mchezaji wa Yanga kwa mujibu wa mkataba.

Hata hivyo taarifa ya TFF imesema uamuzi kamili kwa pande zote mbili zinazohusika katika shauri hilo utatolewa Januari 9, 2023.

Klabu ya Yanga iliwasilisha malalamiko mbele ya kamati hiyo ikipinga hatua ya mchezaji Feisal Salum kuvunja mkataba kati yao bila kuishirikisha klabu.

Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ilisikiliza malalamiko hayo Januari 6 ambapo pande zote mbili (Yanga na Feisal Salum) ziliwakikishwa na wanasheria wao.

Related Articles

Back to top button