Mapinduzi CupNyumbani
Ni vita Mapinduzi Cup leo
MICHUANO ya Kombe la Mapinduzi inaendelea leo kwa michezo miwili visiwani Zanzibar.
Mchezo wa awali, APR itaikabili JKU kisha Simba kuivaa Singida Fountain Gate michezo yote ya kundi B ikifanyika uwanja wa New Amaan.
Tayari Singida Fountain Gate imetinga robo fainali huku Simba ikihitaji ushindi katika mchezo huo kujihakikishia mazungira mazuri.
Katika mechi mbili zilizopigwa Januari 2, Yanga imeichapa Jamus mabao 2-1 mchezo wa kundi C huku Azam iliifunga Vital’o mabao 3-1 kundi A.