Ligi Kuu

Mngqithi awapa maua yao Fountain Gate

ARUSHA: KOCHA Mkuu wa Yanga, Manqoba Mngqithi, amesema amevutiwa na namna wapinzani wao walivyowapa nafasi wachezaji vijana, akisisitiza kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya soka la Tanzania na timu za taifa.

Mngqithi amesema alifurahishwa zaidi kuona kocha wa wapinzani akiwa tayari kuwaamini vijana wengi, akisema hilo linaweza kusaidia kujenga kizazi bora cha wachezaji wa Tanzania.

“Nilivutiwa sana na wapinzani wetu, lakini jambo lililonifurahisha ni kuona kocha ambaye yuko tayari kuwapa nafasi vijana wengi. Mustakabali wa soka la nchi,”amesema baada ya kuibamiza Fountain Gate mabao 2-0 jana.

Tayari Yanga wametua Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Gaborone United utakaochezwa mwishoni mwa wiki hii ugenini nchini Botswana.

Yanga imekuwa ya moto tangu kuanza kwa msimu huu baada ya kucheza michezo mitano ya Ligi Kuu na kushinda yote ikijiweka kileleni mwa msimamo kwa pointi 15, sasa macho ya mashabiki wengi yanasubiri kuona kama ubora wao watauonesha kimataifa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button