Kwingineko

Galatasaray: Osimhen hauzwi

UTURUKI: RAIS wa Galatasaray, Dursun Özbek, amesema klabu hiyo haina mpango wowote wa kumuuza mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen licha ya kuendelea kuvutia vilabu vikubwa vya Ulaya.

Özbek amesema ni jambo la kawaida kwa mchezaji mwenye kiwango kikubwa kama Osimhen kuingia kwenye rada za klabu kubwa, lakini akasisitiza kuwa maslahi ya Galatasaray ndiyo kipaumbele cha kwanza.

Kiongozi huyo amesema Osimhen ana furaha kuendelea kucheza nchini Uturuki na hakuna mpango wa kumruhusu kuondoka katika dirisha la usajili wa majira ya joto.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa na msimu bora akiwa Galatasaray ambapo amefunga mabao 22 na kutoa pasi nane za mabao katika michezo 33, akichangia mabao 30 moja kwa moja.

Kiwango chake kimeisaidia Galatasaray kutwaa ubingwa wa nne mfululizo wa ligi ya Uturuki pamoja na kufika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mafanikio hayo yamevutia vilabu vikubwa barani Ulaya ikiwemo Real Madrid, Barcelona, Paris Saint-Ge

Related Articles

Back to top button