Nyumbani

Patashika Ligi ya Championship leo

LIGI ya Championship inaendelea leo kwa michezo mitano kwenye viwanja tofauti.

Pamba itakuwa mwenyeji wa African Sports kwenye uwanja wa Nyamagana, Mwanza huku Fountain Gate ikiwa mgeni wa Kitayosce kwenye uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.

JKT Tanzania itakuwa wageni wa Mashujaa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma wakati Ndanda ni mwenyeji wa Biashara United kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.

Nayo Green Warriors itaikaribisha Copco kwenye uwanja wa Mej.Jen. Isamuhyo, Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button